Tuesday, December 22, 2015

JINSI YA KUSAFISHA USO

Ungependa kujua jinsi ya Kusafisha uso wako? ?. ■Kusafisha uso ni njia mojawapo ya kuutunza ili kuukinga na ukavu, kuharibika kwa ngozi na athari zingine zote. Lakini tu kumbuka unahitajika kufanya Kwa kutumia njia sahihi maana ukutumia njia zisizo sahihi utakuletea madhara pia.  
■Haijalishi una ngozi kava, laini, au katikati ya hizo ni lazima kusafisha ngozi yako ya usoni hata ukiwa na chunusi. Unachotakiwa kufanya ni kuosha kulingana na aina ya ngozi yako. 
■Leo tutaangalia njia ya kwanza ambayo ni
 1: OSHA USO WAKO KILA SIKU
A: Lowanisha uso wako  na maji ya uvuguvugu, Maji ya moto au baridi sio mazuri maana yanaweza kuharibu ngozi yako. 
•Tumia mikono yako kujiwagia maji usoni au tumia kijitaulo kidogo. Vile upendavyo. Lakini hakikisha mikono yako ni safi ili usiupe uso wako bakteria kutoka mikononi mwako. 
•Pia kumbuka kulowanisha usowako kabla ya kutumia sabuni maalumu ya kuoshea uso kunafanya sabuni kupita kwa urahisi na hivo kutakatisha uso wako vizuri kabisa. 

B: Tumia sabuni maalumu ya kuoshea uso upendayo kulingana na aina ya ngozi yako. 
•Sugua taratibu sana kwa kufanya duara, au mzunguko ukutumia kitaulo maalum kilaini.  Usitumie nguvu nyingi. 
•Epuka kutumia subuni za kuogea au kufulia usoni mwako maana uso una ngozi laini tofauti na mwilini hivo kupata Madhara ni rahisi. 
•Kama ulipaka makeup tumia maji maalumu ya kuondolea makeup au makeup tissue kuondoa makeup usoni kabla ya kuanza kuosha. Vile ukiosha ukiwa na makeup hautata
ka na unaweza kusababisha madhara..

C: Fanyia uso wako scrub
•Fanya scrub kwa kuzungusha kama unavoosha ila yale maeneo yenye ukavu au mafuta Mengi yape kipaumbele zaidi. 
•Sugua uso taratibuu na usitumie nguvu nyingi. Unapomaliza kuosha uso wako ndipo fanya scrub "Tutaongelea siku jinsi ya kufanya scrub".
•Sio lazima kila siku ufanye scrub chagua siku za kufanya labda mara tatu, mbili au moja kwa wiki kutegemeana na uhitaji wa ngozi yako. 
•Unaweza kutumia scrub za asili ipo siku Tutaongelea scrub  za asili. Endelea kuwa nasi. 
 
D: Osha uso wako na uukaushe
•Safisha scrub yote kwa maji ya uvuguvugu kama kawaida hadi uhakikishe umetakata na ukaushe kwa kitaulo laini kwa kuusponge hivi usiukaushe kwa kuusugua maana unaweza ukaupa mikwaruzo au mikunjo. 

E: Paka Toner
•Toner inasaidia kunyoosha ngozi yako na kuziba vijitundu hivo kuifanya ngozi yako Iwe na mng'aro mzuri. Sio lazima kupaka toner unaweza kuruka. Lakini kama unapaka paka ambayo ni aina ya ngozi yako. Kuna toner za asili tutaangalia siku zijazo. 

F: Paka Moisturiser yako
•Moisturiser inasaidia sana kufanya ngozi yako iwe laini na nzuri yenye mng'aro na kuvutia. Inasaidia kuondoa ukavu na mikunjo usoni mwako. 
•Usiku ukipaka itatunza ngozi yako kwa usiku mzima. Kuna ambao hawapakagi lakini angalia na uhitaji wa ngozi yako. 
•Mchana tafuta moisturiser ambayo itakukinga na mionzi ya jua ili kutunza ngozi yako isiharibike. 
■TUTAISHIA HAPA KWA LEO, Tu kufanya wakati mwingine kuangalia Njia ya pili ya uoshaji uso. 
• Ukiwa na swali tafadhali usisite kuuliza kupitia comment's .
Hadi wakati mwingine tena
Sepprise Joseph
GETS-STYLIST.  



No comments:

Post a Comment