Monday, February 08, 2016

JINSI YA KUFICHA TUMBO/ NYAMA ZA TUMBONI

1. VAA HIGH WAIST
Pendelea kuvaa high waist skirt, jeans, trouser au pant. Unapovaa aina hii ya nguo itakufanya ufiche tumbo lako na kukuonesha mwembamba maana pale unapovalia nguo juu ni pembamba zaidi kuliko kiunoni. Kila kitu kitafichwa. Na low waist itakukata na kukuonesha tumbo lako.

2. VAA SHAPE WEAR
Tafuta shape wear nzuri na imara ambayo itakufanya mwili wako ukae vizuri kuanzia kwenye mapaja hadi kifuani. shape wear ni nzuri kuliko corset maana corset kama una nyama nyingi itakukata nyama na zitaonekana badala ya kukuziba na upendeze unapovaa.

3. VAA BLOUSE PANA PANA
Blouse pana hazishiki sana mwili hivo zitakufanya usionekane tumbo lako. Blouse kama za peplum zinafaa sana kuficha tumbo lako.epuka kuvaa nguo zitakazokuchoresha tumboni..

4. BLAZER
Pendelea kuvaa blazer, shrugs au kitupio chochote juu ambacho kitakusaidia sana kuficha tumbo lako lisionekane na ukaonekana umependeza zaidi.